DJ Seven amvaa Harmonize kwa kumchukua Poshy Queen

Celebrity Trending
By -
0

 

Download The world news app and enjoy additional content


Mzozo wa kimapenzi kati ya msanii wa Bongo Flava, Harmonize, na aliyekuwa DJ wake, DJ Seven, umechukua sura mpya baada ya video ya Harmonize na Poshy Queen kuibuka mtandaoni.

Video hiyo inaonesha Harmonize na Poshy Queen wakiwa kwenye boti wakifurahia maisha. Poshy Queen ni mrembo mwenye umbo la kuvutia ambaye alikuwa akihusishwa na DJ Seven kimapenzi.

DJ Seven, ambaye alitengana na Harmonize kikazi hivi karibuni, alijibu kwa kurepoat video hiyo kwenye insatastory yake na kuandika: “Stop tagging me on those nonsense waambieni waende hata Maldives.” Hii inaashiria kuwa DJ Seven anaonekana kuwa na uchungu kwa kumpoteza Poshy Queen kwa Harmonize.

Harmonize, ambaye anajulikana kama Konde Boy, aliamua wakosane na DJ wake kisa Poshy Queen, kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo. Harmonize alikuwa na uhusiano na mwigizaji Kajala Masanja kabla ya kumwagana naye kwa madai ya kumdanganya na binti yake, Paula Kajala.

Poshy Queen amepost picha ya Harmonize kwenye instastory yake na kuonesha kuwa wako kwenye penzi zito. Wawili hao wamepokea maoni mbalimbali kutoka kwa mashabiki wao, wengine wakiwatakia heri na wengine wakiwakosoa.

Tags:

Post a Comment

0Comments

Post a Comment (0)